Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, limekamata silaha tano na
risasi 12, katika pori la vikindu, zikiwa zimetelekezwa kufuatia
operesheni maalumu ya siku saba.
Operesheni
hiyo ililenga kukamata magari ya wizi, majambazi, wauzaji wa dawa za
kulevya, wauza gongo na makosa ya usalama barabarani.
Mbali
na hilo, operesheni hiyo imefanikiwa kukusanya sh. 215,090,000,kutokana
na makosa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia januari 13 mpaka 15,
mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon
Sirro.Amesema kuwa wamefanya operesheni hiyo katika pori la vikindu,
Mkoani Pwani kufuatia ongezeko la matukio ya uhalifu katika maeneo
mbalimbali ya Dar es salaam.
Aidha,
Sirro amesema kuwa watuhumiwa 362, walikamatwa na makosa mbalimbali na
kuongeza kuwa wamekamata silaha aina ya SMG moja, shortgun mbili na
bastola mbili.
Hata
hivyo, Sirro amesema kuwa katika operesheni hiyo imebainisha maeneo
yaliyokithiri kwa matukio ya uhalifu ni Kigogo Freshi na Yombo Vituka.
No comments:
Post a Comment