Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
tarehe 17 Januari, 2017 amemteua Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma kuwa Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.
Kabla
ya kuteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji
Prof. Ibrahim Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Mhe.
Jaji Prof. Ibrahim Juma atakaimu nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania mpaka
hapo Mhe. Rais Magufuli atakapofanya uteuzi wa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Uteuzi wa Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Januari, 2017
No comments:
Post a Comment