Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.
Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Abdallah
Bulembo ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazzi wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), na pia alikuwa ni mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kabla ya
majukumu ya kuendesha kampeni za urais mwaka 2015 zilizomuingiza Rais
Magufuli madarakani.
Kwa
upande wake Prof Kabudi, ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Kitivo cha Sheria, lakini kilichong'arisha zaidi ni pale alipoteuliwa na
Rais Kikwete kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya na
Kuratibu Maoni ya Katiba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mst.
Joseph Sinde Warioba.
Prof. Kabudi amekuwa mahiri katika mihadhara mbalimbali kitaifa, hasa wakati ule wa mchakato wa Katiba Mpya.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa.habarimpekuzihuru
No comments:
Post a Comment