Mwanamke
mmoja aliyejulikana kwa jina la Anastazia Francis miaka 48 amekutwa
akiwa amejinyonga hadi kufa katika mtaa wa Nyasaka wilaya ya Ilemela
jijini Mwanza.
Taarifa
ya jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imesema kuwa mnamo tarehe 16.01.2016
majira ya saa 11:00 asubuhi, mwanamke huyo alikutwa akiwa amejinyonga
hadi kufa ndani ya chumba chake kwa kutumia mtandio ambao alikuwa
ameuning’iniza kwenye dirisha juu.
Inadaiwa
kuwa mwanamke huyo baada ya mumewe kuondoka alimtuma mwanae mkubwa
aliyemaliza kidato cha nne aende dukani na mwingine mdogo mwenye umri wa
miaka 06 aende kufagia na ndipo alipopata mwanya wa kwenda kujinyonga
hadi kufa.
Tukio
hilo lilijulikana baada ya mtoto wake mdogo kurudi ndani chumbani
kuchukua shati na kumkuta mama yake akiwa amejining’inizi ndipo aliita
watu ili waje kumsaidia.
Taarifa hiyo ya jeshi la polisi imesema kuwa upelelezi unaendelea ili kufahamu chanzo cha tukio hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amewaasa wananchi pindi
wanapopata matatizo waombe ushauri kwa watu wengine ili kuweza kuepusha
maamuzi ambayo ni hatari katika maisha yao.habari na mpekuzi huru
No comments:
Post a Comment